MAGONJWA YA UYOGA NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO

MAGONJWA YA UYOGA NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO

Mavuno duni husababishwa na mojawapo ya mambo yafuatayo

Mbegu isiyo bora au iliyoingia uchafu, mbegu change mno au iliyokomaa kupita kiasi si nzuri.

Ubora wa vimeng’enywa . virutubisho na uwezo wa kunyonya maji.

Hali ya joto .Joto kali mno huua vijikivu.

Ukosefu wa unyevu kwenye hewa ukosefu wa hewa safi na ufinyu wa mwanga.

Wadudu na magonjwa.

Wadudu na Wanyama hula mbegu na kueneza vichafuzi (contaminants). Hivi hushindania virutubisho na vijiuzikuvu, pia hutoa sumu ambazo huua vijiuzikuvu. Wadudu kama minyoo na konokono na Wanyama kama panya hula mbegu pamoja na matunda ya uyoga. Nzi hasa wale wadogo (fruit flies au Drosophilla) hutaga mayai ambayo huanguliwa lava ambao hula vijiuzikuvu na matunda.

Kuzuia au kukabiliana na magonjwa.

Matatizo ya magonjwa kwenye uyoga hutokana na uangalizi usioridhisha wa banda au kutotayarisha vimeng’enywaa vizuri aua kutumia mbegu iliyochafuliwa.

Hatua za kuchukua

Kabla ya kulitumia banda

Lisafishe na maji yenye Dettol au sabuni.

Pakaa chokaa kwenye kuta, chaga, madirisha na sakafu siku mbili kabla ya kuotesha.

Acha chumb kikauke.

 

Wakati wa kuotesha

Weka dawa mlangoni au tumia viatu maalumu.

Weka nyavu madirishani kuzuia wadudu wasiingie.

Wakati wa kuvuna anza na mifuko safi ndipo uendelee na ile iliyoathirika au ya zamani.

Hakikisha chumba ni kisafi saa zote.

Vimeng’enywa vilivyotumika viwekwe mbali na banda na vile vilivyoathirika na magonjwa vichomwe moto.

Matunda yote yaliyoharibika na yale yaliyoshindwa kukua pamoja na vishina viondolewe kila wakati wa kuvuna ili visivutie wadudu.

Usiguse mifuk au matunda yaliyoathirika wakati wa kuvuna . Yakusanye mara baada ya kuvuna yatupe mbali.

 

Magonjwa mwngine na namna ya kuyazuia.

Haya ni yale yanayosababishwa na virusi, bacteria na kuvu.

Virusi

Magonjwa ya virusi husambazwa na mbegu (spores) au vijuzikuvu (mycelium)

Namna ya kuzuia

Ikiwezekana uyoga uvune kabla haujachanua (hii inawezekana tu kwa uyoga aina ya Agaricus).

Badilisha aina ya uyoga unaolima na kulima aina nyingine.

 

Bacteria

Hawa utawajua kwa kuona vitu kama ute mweupe kwenye vimeng’enywa na sehemu nyingine vijiuzikuvu havitandi. Hutoa harufu mbaya ya ammonia.

Namna ya kuzuia usienee

Ondoa mifuko iiyoathirika na itupe mbali. Baada ya msimu wa mavuno safisha banda kwa mvuke au dawa (Dettol). Waweza kutumia 150ml za hypochlorite asilimia 10 kwenye lita mia za mjai.

 

Kuvu (fungi)                                                                      

Hawa huonekana kama vijiuzikuvu dhaifu vinavyokua na kutoa mbegu mapema mno. Mara nyingi huwa na rangi za kijani au nyeusi. Ukitumia dawa waweza kusababisha kutokezea aina ambayo itakua sugu kwa dawa. Mashamba haya ya tengwe na kuchomwa moto.

 

Wadudu wanaoshambulia uyoga

Hawa ni kama nzi aina ya Drosophila ambao hula vijiuzikuvu (mycelium) na kutaga mayai kwenye matunda.

Namna ya kuzuia

Zingatia usafi dawa za kawaida za kuua nzi majumbani zaweza kutumika.

ANGALIZO:  Madawa ni hatari kwa afya za watu. Hivyo inashauriwa kuzingatia usafi w abanda kuliko kuruhusu magonjwa yatakayopelekea kutumia madawa!.

 

Je; umewahi kusumbuliwa na wadudu katika shamba lako? kama ndio ni njia gani uliyoitumia kupambana nao?

WASILIANA NASI +255765264666