KILIMO CHA UYOGA KIGOMA, TANZANIA
MAHITAJI YA KILIMO CHA UYOGA.pdf
JINSI YA KUANDAA KIMENGENYWA.pdf
FOMU-YA-MKULIMA-WA-UYOGA-TAASISI-YA-UYOGAPLUS.pdf
HATUA ZA UOTESHAJI WA UYOGA MAMAMA (Oyster mushroom). pdf
Wakazi wa mkoa wa Kigoma maeneo ya Kibondo, Mvugwe na kambi maalum za wakimbizi (NDUTA NA NYARUGUSU REFUGEE CAMP), wamehamasika sana kulima uyoga baada ya kupata mafunzo kwa vitendo kutoka wataalamu wa kilimo cha uyoga chini ya taasisi ya Uyogaplus.
Akina mama wameonekana kufurahishwa Zaidi na kilimo cha uyoga, wamekua wakitembea umbali mrefu kutafuta aridhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo. Kilimo cha uyoga hakitumii udongo hivyo haki athiriwi na ukosefu wa rutuba kwenye udongo, pia ni kilimo cha nyumbani kinacho jali usafi mama nyumbani anaweza kuotesha uyoga na kulea Watoto bila tatizo. Sehemu mbalimbali Tanzania hasa vijijini mashamba makubwa yana milikiwa na wanaume, wanawake wanamiliki kidogo na wengine hawamiliki kabisa, kilimo cha uyoga ni mkombozi kwa mwanamke kwa kua hakihitaji eneo kubwa aridhi kama ilivyo mazao mengine.
Faida za kilimo cha uyoga
Kupata chakua bora kwa mwaka mzima bila kusubiri msimu wa mvua
Ajira kwa wazee, kinamama na vijana kwani kinahitaji mtaji mdogo na mazao hupatikana katika mda mfupi.
Kilimo hiki ni salama kwa kiafya na kimazingira kwani hakitumii viuatilifu (pesticides).
Kupunguza uchafu wa mazingira kwa kutumia takatakka.
Mabaki ya takataka iliyo limwa uyoga (vimenge’nywa) ni chakula bora kwa mifugo n ani mbolea nzuri.
Kupata uyoga wenye virutubisho muhimu kwa kulima uyoga wenye masalia ya mimea kama vile mwani ambao una kiasi kikubwa cha madini joto.
Kupunguza matukio ya vifo vitokanavyo na kula uyoga wenye sumu.
Kilimo cha uyoga ni rahisi na pia kinahitaji mtaji mdogo wa kuanzia. Hivyo kilimo hiki kinawez pia kikatekelezwa na wakulimwa wadogo wadogo waishio vijijini ambao kipato chao ni kidogo. Kwa vile uyoga unaweza ukalimwa kwa mwaka mzima ukilinganishwa na mazao kama maharage, uzaaji wake ni mkubwa. Jambo linguine muhimu ni uwa kilimo cha uyoga hakiharibu mazingira, kwani uyoga hulimwa ndani ya mabanda, kwhyo hakuna matatizo ya mmomonyoko wa udongo. Kisha baada ya mavuno masalia yaliyobaki yanawza kurutubisha ardhi au kulishia mifugo. Faida nyingine ya kilimo cha zao hili linaweza kutumika kama zao la biashara. Kilo moja ya uyoga mbichi huuzwa kati ya Sh 5,000 na Sh 10,000. Soko la ndani ya nchi bado ni nzuri kwa vile hakuna wazalishaji wengi wa uyoga pia uwezekano upo wa kusafirisha nje kama uzalishaji utaongezeka na mikakati Madhubuti itatengenezwa. Nchi kama Afrika kusini, Zibabwe, Kenya hujipatia fedha za kigeni kwa kuuza uyoga nje ya nchi zao. Korea ya kusini hujipatia kila mwaka dola za kamarekani 600 miioni kutokana na mauzo ya aina ya Ganoderma, Thailand huuza nje kila mwaka uyoga wenye thamani ya dola za kimarekani 60 milioni.