KILIMO CHA UYOGA TANZANIA

KILIMO CHA UYOGA TANZANIA

MAHITAJI YA KILIMO CHA UYOGA.pdf

JINSI YA KUANDAA KIMENGENYWA.pdf

FOMU-YA-MKULIMA-WA-UYOGA-TAASISI-YA-UYOGAPLUS.pdf

UTANGULIZI

Uyoga ni mmea aina ya kuvu (fungi) unaotofautiana na mimea mingine kwa kukosa umbijani(chlorophyll) inayouwezesha kujitengenezea chakula wenyewe kwa kutumia hewa ya ‘carbon dioxide’ na mwanga (photosynthesis). Hutumia chakula kilichotengenezwa tayar na mimea au Wanyama. Kwa mfano, uyoga wa kienyeji huota wenyewe mashambani na msituni hasa wakati mvua imeanza kunyesha kukiwa na masalia ya mazao ya msimu uliopita. Uyoga hutoa dawa zinazoitwa vimenge’enyo (enzymes) zenye uwezo wa kuyeyusha au kusaga (degrade) masalia ya mazao ya kilimo (organic matter) ili kujipatia chakula chake.

 

Faida za uyoga

Sehemu nyingi za Tanzania zinakabiliwa na matatizo ya utapiamulo hasa Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Uyoga ua viini lishe vingi kama vile protini (19-40%), Vitamini A,B,C,D na K, na madini ya aina ya phosphorus, chuma na potash kwa kiasi kikubwa. Kwahyo uyoga ukitumiwa kama chakula unawezakupunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya utapiamulo.

 

Vilevile uyoga una kiasi kidogo cha mafuta ya na hauna lehemu (cholesterol0 ambayo husababisha madhara katika mishipa ya damu. Badhi ya aina za uyoga kama Ganoderma lucidum, Lentinular edodes, Trimella fuciformis na nyinginezo huweza kusaidia, shinikizo la damu, aina mbalimbali za saratani, moyo, kifua kikuu, figo na kuchochea kinga ya mwili.

 

Tanzania inao urithi mkubwa wa uyoga wa asili ambao unaota porini na mashambani. Kati ya uyoga huu kuna ule wenye sumu. Ulaji wa uyoga wenye sumu unahatarisha Maisha ya binadamu. Mara kwa mara tumesikia watu wame lazwa hospitalini au hata kufa kwa kula uyoga usiofaa (wenye sumu). Katika sehemu nyingi za Tanzania hasa wakati wa mvua, wenyeji huokota uyoga kutoka porini au mashambani na kwenye vichuguu kwa matumizi ya nyumbani kama chakula. Kwa vile uyoga unaota porini na mashambani wakati wa mvua tu, basi familia nyingi hukausha uyoga kwa matumizi ya baadaye. Hii inaonesha umuhimu wa uyoga kama mboga.

 

Kutokana na uharibifu wa mazingira unaondelea nchini kama vile misitu kufyekwa au kuchomwa moto, uyoga wa asili umeendelea kuadimika. Teknolojia ya kuzalisha uyoga  inatuwezesha kupata uyoga bila kwenda kuutafuta porini.

 

Faida za kilimo cha uyoga

Kupata chakua bora kwa mwaka mzima bila kusubiri msimu wa mvua

Ajira kwa wazee, kinamama na vijana kwani kinahitaji mtaji mdogo na mazao hupatikana katika mda mfupi.

Kilimo hiki ni salama kwa kiafya na kimazingira kwani hakitumii viuatilifu (pesticides).

Kupunguza uchafu wa mazingira kwa kutumia takatakka.

Mabaki ya takataka iliyo limwa uyoga (vimenge’nywa) ni chakula bora kwa mifugo n ani mbolea nzuri.

Kupata uyoga wenye virutubisho muhimu kwa kulima uyoga wenye masalia ya mimea kama vile mwani ambao una kiasi kikubwa cha madini joto.

Kupunguza matukio ya vifo vitokanavyo na kula uyoga wenye sumu.

Kilimo cha uyoga ni rahisi na pia kinahitaji mtaji mdogo wa kuanzia. Hivyo kilimo hiki kinawez pia kikatekelezwa na wakulimwa wadogo wadogo waishio vijijini ambao kipato chao ni kidogo. Kwa vile uyoga unaweza ukalimwa kwa mwaka mzima ukilinganishwa na mazao kama maharage, uzaaji wake ni mkubwa. Jambo linguine muhimu ni uwa kilimo cha uyoga hakiharibu mazingira, kwani uyoga hulimwa ndani ya mabanda, kwhyo hakuna matatizo ya mmomonyoko wa udongo. Kisha baada ya mavuno masalia yaliyobaki yanawza kurutubisha ardhi au kulishia mifugo. Faida nyingine ya kilimo cha zao hili linaweza kutumika kama zao la biashara. Kilo moja ya uyoga mbichi huuzwa kati ya Sh  5,000 na Sh 10,000. Soko la ndani ya nchi bado ni nzuri kwa vile hakuna wazalishaji wengi wa uyoga pia uwezekano upo wa kusafirisha nje kama uzalishaji utaongezeka na mikakati Madhubuti itatengenezwa. Nchi kama Afrika kusini, Zibabwe, Kenya hujipatia fedha za kigeni kwa kuuza uyoga nje ya nchi zao. Korea ya kusini hujipatia kila mwaka dola za kamarekani 600 miioni kutokana na mauzo ya aina ya Ganoderma, Thailand huuza nje kila mwaka uyoga wenye thamani ya dola za kiarekani 60 milioni.

MAHITAJI YA KILIMO CHA UYOGA

Mpira (pvc pipe) wan chi mbilimbili ukatwe vipande vya sentimeta mbili kila kimoja (collars)

Kamba ya katani

Mifuko ya plastiki inatostahimili joto

Mpira wa manati

Vimengenywa

Kiloba kwa ajili ya kulowekea vimeng’enywa

Pipa la lita 240 la kuchemshia vimeng’enywa

Pipa au Karo la kulowekea vimeng’enywa

Pumba ya mpunga au ya mahindi, sukari na chokaa au jasi kwa ajili ya kuongeza virutubisho (ziada)

 

Vimeng’enywa.

Vimeng’enywa bora ni vile vyenye uwezo wa kushika maji kiasi na ambavyo kwavyo vijikuvu vitatanda bila matatizo. Visiachane sana na wala visishiakamane sana. Vimeng’enywa sharti view vimekauka kwani uyoga hauoti kwenye vimeng’enywa vyenye rangi ya kijani.

Masalia ya mazao ya kilimo karibu yote yanafaa, kwa mfano masalia ya mahindi (mabua na magunzi), ngano, mtama, mpunga, ulezi, masalia ya jamii ya kunde kama maharage, kunde, soya n.k na pia mazao mengine kama migomba , pamba, katani n.k. mabaki ya viwandani kama vile mabaki ya mimea toka viwanda vya pombe, makapi ya mbegu za mafuta, miwani, magugu maji, na kadhalika.

Mbegu za uyoga

Mbegu ya uyoga yaweza kutengenezwa kwa kutumia nafaka, mabaki ya mbegu za nafaka, vumbi la mbao nk. Mbegu husambazwa ikiwa ndani ya chupa ya kioo ikiwa imeandikwa aina ya mbegu tarehe ambayo mbegu imetengenezwa . Mbegu itakua nzuri kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kutengenezwa. Inafaa mbegu itunwe kwenye kivuli haipendi jua. Kama hauko tayari kupanda basi inabidi utunze kwenye jokofu 96-10⁰C) ambako inaweza kukaa kwa mda wa miezi 2. Baada yah apo mbegu hupoteza ubora wake. Hakikisha unanunua mbegu kutoka katika maabara za taasisi zenye wataalamu.

KWAMAHITAJI YA MBEGU BORA ZA UYOGA KWA BEI NAFUU PIGA +255765264666

 

Banda la kuoteshea uyoga

kawaida uyoga huoteshwa ndani y abanda. Banda laweza kuwa la matofali au udongo paa huezekwa kwa kutumia nyasi kwasababu bati  mabadiliko ya hali ya joto kati ya mchana na usiku. Kwa mkulima mdogo banda lenye ukubwa wa mita 5×8 linatosha . Banda linatakiwa kugawanywa katika vyumba viwili. Chumba  kimoja kidogo kisicho na madirisha asipokuwa mlango wa kuingilia.Chumba hiki chenye giza hutumika kuuzia uyogakabla ya kuanza kutoa matunda. Uyoga hupenda kukua kwenye giza na joto. Chumba cha pili kinatakiwa kua na madirisha makubwa yaliyofunikwa kwa wavu wa kuzuia mbu ili kuzuia wadudu wasiingie. Miango y abanda inatakiwa iwe imefungwa mda wote hasa ile ya chumba cha giza. Kama unatumia chumba kimoja tu basi wakati uyoga unatanda utengenezee giza ama kwakufunika nguo nyeusi au kwa kusia mbegu kwa kuzichimbia katikati ya mfuko.

Mifuko ya plastiki

Uyoga hupandwa kwenye mifuko ya plastiki inayostahimili joto. Ukubwa wa mifuko inayofaa ni ile inayoweza kuchukua kiasi cha kilo 3-4 za vimeng’enywa vinyevu kwa sehem za baridi. Kwa sehemu za joto kama Dar es Salaam, mifuko iwe midogo kiasi cha kuingia kilo 1-2 za vimeng’enywa.

 

Kutayarisha vimeng’enywa

 

Katakata (kama ni lazima) na loweka vimeng’enywa.

Muda wa kuloweka unatofautiana kulingana na uwezo wa vimeng’enywa kunyonya maji, baadaye chuja maji. Changanya chokaa (1%) na sukari (1-2%) kwanza kisha changanya na pumba (20% ya vimeng’enywa vikavu). Weka mchanginyiko huu kwenye vimeng;enywa na changanya vizuri. Tumia mifuko inayostahumili joto.

Toboa mfuko upande wa pili kisha funga kwa kamaba ya katani.

Jaza vimeng’enywa kisha funga tena juu kwa Kamba ya katani.

Chemsha kwa mvuke kwa masaa 4 kisha acha ipoe kwa mda wa masaa 12 hadi 24.

 

Kupanda

Fungua upande mmoja, sambaza mbegu juu kisha funga.

Fungua upande wa pili na ufanye vivyo hivyo.

Waweza kuipanga mifuko kwenye vichanja ndani ya chumba cha giza au kuifunika kitambaa cheusi.

Wakati wa kuzalisha uyoga ukifika fungua mifuko, ivalishe kola/shingo na iweke mifuko katika mazingira ya kuzalisha (cropping).

Njia hii ya kulima uyoga ni nzuri na yaweza kureebishwa kufuatana na uwezo  au mapendekezo ya mlimaji. Kwa mfano badala ya kuivalisha mifuko kola waweza kuifunga kwa kaba na wakati wa kuzalisha (fruitification) unapowadia unakata matundu pande mbili za mifuko au unachanachana kwa kisu kuruhusu uyoga kutoka.

Uwiano wa mbegu na vimeng’enywa

Uwiano wa mbegu na vimeng’enywa ni moja ya mambo yanayoathiri mavuno ya uyoga

Kiasi kidogo mno cha mbegu huchelewesha kutanda kwa vijiuzikuvu kwenye vimeng’enywa. Pia hurahisisha uyoga kushambuliwa na vijidudu (contaminants).

Kiasi kikubwa mno cha mbegu hufanya vijizikuvu kutanda haraka na hivyo kushinda vijidudu. Hata hivyo hii inaweza kusababisha mavuno duni kwani virutubisho kwenye vimeng’enywa huisha kabla ya uyoga haujaanza kuzaa.

Kiasi cha asilimia 1.5 kinapendekezwa . hii ikiwa na maana kuwa kwa kilo moja ya vimeng’enywa vilivyo tayari tumia mbegu kiasi cha gram 15. Chupa moja ya mbegu ina kiasi cha grau 150-180. Hivyo kwa chupa moja waweza kuotesha mifuko 10-15 ya kilo mojamoja.

Kukuza uyoga -kuvundika (incubation)

Baada ya kupanda mifuko ipelekwe kwenye chumba cha giza cha kukuzia ambacho kina giza. Kiasi cha giza ni kie kitakachomfanya mtu ashindwe kusoma gazeti. Kma huna chumba ambacho kina giza unaweza kutumia bosi lililofunikwa au waweza kufunika na kitambaa cheusi . Mifuko itakaa kwenye giza kwa mda wa siku 20-30 kutegemeana na aina ya uyoga na hali ya joto. Kama mazingira si mazuri ndani ya mifuko, uyoga huu unaweza kuchelewa kuzaaa hadi kufikia miezi miwii.

Uyoga aina ya mamama (oyster mushroom) unaweza kulimwa kwenye joto la 15-30⁰C ila hustawi vizuri Zaidi kwenye joto la wastani (20-25⁰C)

Mambo mengine ya kuzingatia

Meza pamoja na vifaa vingine vya kuoteshea vinapaswa kusafishwa vizuri na Dettol au spirit ili kupunguza uwezekano wa vimeng’enywa kuchafuliwa wakati wa kupanda.

Hakikisha unapata mbegu bora kutoka kwa wataalamu wa kuzalisha mbegu. Mbegu nzuri ina utando mweupe uliofunika ile nafaka na ina harufu nzuri ya uyoga. Rangi nyeusi na za kijani ni dalili ya uchafu. Harufu mbaya pia ni dalili ya mbegu chafu.

Ni vizuri banda lijengwe kwenye kivuli kupunguza joto la jua.

Hakikisha banda linakua safi saa zote.

Banda lisiwe na Nyanja za kuingiza panya, wadudu na kadhalika.

 

Kuotesha uyoga (fruitification/cropping)

Baada ya vijiuzikuvu kutanda kwenye mfuko wote dalili za uyoga huanza kuonekana kama tupunje tudogo sana ndani ya mifuko.

Mifuko sasa ihamishwe kwenye chumba cha kuzalishia chenye mwanga wakutosha.

Kisu kisafi kitumike kuchanja mifuo kuruhusu hewa na unyevu kuingia.

Ili uyoga uzae unahitaji ubaridi, unyevu na hewa ya oksijeni Zaidi kuliko wakati wa kukua.

Mwanga ni muhimu sana kwa uyoga ili uzae.

Ili kushusha kiwango cha joto ndani y abanda na kupandisha kile cha unyevu, maji ya mwagwe kwenye sakafu na ikibidi kwenye kuta.

 

 Uvunaji.

Wakati wa kuvuna shika shina la uyoga kwa vidoel na kuzungusha polepole huku ukiwa unavuta, usitumie kisu. Hakikisha shina halibaki kwenye shimo hii itazuia uyoga mwingine kuota pia itavuia vijidudu ambavyo huzuia uyoga mwingine usitoe. Wakati wa kiangazi kwa vile unyevunyevu kwenye hewa ni mdogo unashauriwa kutundia magunia yenye maji katika banda la uyoga au mwaga maji kwenye sakafu na kunyunyiza maji kwenye mifuko. Kama mfuko utaonekana unakauka pia uyoga unaoota unakauka basi tumbukiza mfuko kwenye ndoo ya maji ili ulowane. Hata hivyo hii ni hatari kwani kama kuna mfuko wenye uchafu utaambukiza wenzake kwa urahisi.

Mavuno

Mavuno utakayopata hutegemeana sana na aina ya masalia ya mazao uliyotumia aina ya mbegu, kiwango cha usafi na mazingira uliyokuzia na kuoteshea. Kwa kawaida kiwango cha mavuno kitakuwa asilimia 70-120% wa uzito wa vimengenywa vilivyotumika.

 

Ufungashaji

Uyoga ukishavunwa ni vyema utumike kabla haujapoteza ubora wake. Kma uyoga hauuzwi mbali mno nae neo la uzalishaji basi mifuko laini ya plastiki yaweza kutuika. Iwapo unauza kwenye maduka ya kisasa au mahoteli waweza kushauriwa na wanunuzi namna ya kufungasha ikiwepo ile ya kufunga kwenye visahani maalumu na kufunika na karatasi maalumu.

KWA MAHITAJI YA UYOGA BONYEZA LINK⇓

https://uyogaplus.com/oyster-mushroom-1-kg-58